Kenya imejikuta kwenye hali ya tahadhari baada ya kifo cha kwanza kinachohusishwa na virusi vya Ebola kutangazwa katika taifa hilo. Rais William Ruto ameeleza kuwa serikali imeanzisha hatua maalum za kulinda raia na kuhakikisha ugonjwa huo hauenei zaidi.

Marehemu, ambaye ni Mkenya aliyekuwa akiishi Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, alisafiri hadi Nairobi kupitia Uganda, hali ambayo imezua mchecheto kuhusiana na ufuatiliaji wa ugonjwa huo. Hatua za dharura zimewekwa katika viwanja vya ndege na vituo vya mipakani ili kuhakikisha hamna uwezekano wa maambukizi ya ziada.